Juma Kaseja kuipa KMC mtelezo kwa Yanga

Alhamisi , 12th Mar , 2020

Klabu ya KMC inatarajia kushuka dimbani leo dhidi ya mabingwa wa kihistoria nchini Tanzania, Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara.

Juma Kaseja

Kuelekea mchezo huo, Kaimu Mtendaji Mkuu wa klabu ya KMC, Walter Harrison amesema kuwa timu yake imejiandaa vizuri kutoa ushindani dhidi ya Yanga kutokana na kujiamini kwa wachezaji wake.

"Katika mechi mbili za mwisho timu yetu imepata matokeo, dhidi ya Mbao FC na JKT Tanzania, kwahiyo sasahivi wachezaji wanajiamini kuelekea mchezo wa leo", amesema Walter.

Kuhusu urejeo wa mlinda mlango Juma Kaseja, Walter Harrison amesema, "Kaseja bado yupo majeruhi lakini anakaribia kurudi langoni. Hajaanza mazoezi pamoja na timu, wiki za hivi karibuni atarejea rasmi lakini atakuwepo kwenye benchi la ufundi katika mechi zetu kutoa hamasa kwa wachezaji".

KMC ipo katika nafasi ya 18 ya msimamo wa ligi, ikiwa na jumla ya pointi 27 katika michezo 27 huku Yanga ikiwa katika nafasi ya tatu na pointi 50.