Alhamisi , 9th Jul , 2020

Winga wa klabu ya Yanga, Juma Mahadhi amesema kuwa ni faraja kwao kuona mchezaji Bernard Morrison anarejea katika kikosi chao kutokana na umuhimu wake.

Juma Mahadhi na Bernard Morrison

Akizungumzia suala la mgogoro wa Morrison na viongozi wa Yanga na urejeo wake, Mahadhi amesema kuwa mambo hayo ni ya kawaida hasa kwenye michezo lakini kikubwa ni furaha yao kumuona akirejea.

"Ni kawaida tu kwamba kuna mambo huwa yanatokea lakini kama viongozi wameamua kukaa na kuamua mambo yaendelee sawasawa ni kitu kizuri", amesema Mahadhi.

"Yaliyotokea ni mambo yake binafsi, sisi kurudi wkake tunamshukuru Mungu kwa sababu ni mchezaji muhimu na tunamtegemea uwanjani", ameongeza.

Kuelekea mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho unaotarajiwa kupigwa wikiendi hii, Mahadhi amesema, "mechi itakuwa ni ngumu sana lakini sisi kwa upande wetu mechi tunaitaka na lazima tushinde kwa uwezo wa Mungu".

Mtazame zaidi hapa.