Jumatano , 22nd Jan , 2020

Aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo na Mbunge wa Chemba), Juma Nkamia amependekeza kujengwa kwa sanamu la Mbwana Samatta, katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, iwe kumbukumbu ya mafanikio aliyoyapata kwa kuwa Mtanzania wa kwanza kuchezea Ligi Kuu ya Uingereza

Mbunge wa Chemba Juma Nkamia na Mbwana Samatta

katika Klabu ya Aston Villa.

Nkamia ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na EATV na EA radio Digital iliyotaka kufahamu kuhusiana na namna ambavyo angetamani Tanzania imkumbuke vipi Mbwana Samatta

Nkamia amesema kuwa "mimi kwangu sio tatizo kujengwa kwa sanamu la Mbwana Samatta hata pale nje ya Uwanja wa Taifa, tena naamini hatua hiyo itakuwa kubwa sana kwake, na heshima kubwa sana kwa Taifa na naamini itakuwa chachu kwa vijana wanaochipukia

Tazama mahojiano kamili hapo chini.