Jumatatu , 9th Jan , 2017

Klabu ya Juventus ya Italia, imejiwekea rekodi mpya ya kushinda michezo 26 mfululizo kwenye uwanja wa nyumbani katika Ligi ya Serie A, baada ya kuifunga Bologna kwa mabao 3-0.

 

Gonzalo Higuain alifunga mabao mawili, huku bao lingine likifungwa na Paulo Dybala, na kuifanya Juve kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi na mahasimu zao, AS Roma.

Juventus, maarufu kama Kibibi kizee cha Turin imedhamiria kuweka rekodi ya kushinda ubingwa wa Scudetto, kwa mara sita mfululizo, huku ikiwa ina mchezo mmoja mkononi.