Ijumaa , 19th Apr , 2019

Kiungo wa klabu ya Chelsea, Ng'olo Kante, ambaye ameisaidia klabu yake kufuzu hatua ya nusu fainali ya Europa League, amesema haamini kama klabu yake ni moja ya timu zinazopewa vipaumbele vya kushinda ubingwa huo.

Ng'olo Kante akiwa na mchezji wa

Kante ambaye ameiita timu yake "underdog" akimaanisha kuwa ni timu isiyopewa kipaumbele kati ya timu nne zilizofuzu hatua hiyo, ambazo ni Arsenal, Valencia na Eintracht Frankfurt.

Chelsea imefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya Europa League baada ya kuiondoa Slavia Prague ya Jamhuri ya  Czech kwa jumla ya mabao 5-3, ambapo sasa itapambana na Eintracht Frankfurt ya nchini Ujerumani.

"Kitu muhimu zaidi ilikuwa ni kufuzu, tunakwenda katika nusu fainali tukiwa tunajiamini na tukiamini kuwa tunaweza kufuzu fainali. Lilikuwa ni lengo letu", amesema Kante alipokuwa akiuzungumza baada ya mchezo huo.

"Hatuna nafasi kubwa ya kushinda ubingwa, tumecheza mechi nzuri hapa (mjini Prague) na tutafanya kila namna tuweze kufuzu fainali lakini hatuna nafasi kubwa ya kushinda", ameongeza.

Bonyeza video hapa chini kutazama zaidi.