Kauli mbiu ya Simba Klabu Bingwa Afrika 2019/2020

Jumanne , 16th Apr , 2019

Afisa Habari wa Simba, Haji Manara amewashukuru mashabiki wa klabu hiyo kwa hamasa yao katika kuhakikisha wanafanya vizuri katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika msimu huu.

Haji Manara na mashabiki wanaoishangilia Simba

Ameyasema hayo ikiwa ni siku chache baada ya kuondolewa na TP Mazembe katika michuano hiyo kwa jumla ya mabao 4-1, katika hatua ya robo fainali.

Manara amesema mashabiki na wanachama ndio walioisaidia kwa kiasi kikubwa Simba kufikia hatua hiyo, kwani waliisaidia Simba kushinda mechi tano za nyumbani.

"Mimi niseme 'very clear' nyuma ya mafanikio haya ni wanachama na mashabiki, bila ya wao kutusaidia tusingeweza kufika hapa. Wametupa nguvu ya dua na sapoti kwani tumeshinda mechi tano za nyumbani bila kupoteza", amesema Manara.

Aidha Manara amesema kuwa mipango yao msimu ujao ni kuvuka hatua ya robo fainali ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika kwakuwa anaamini Simba wataibuka mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Bonyeza hapa chini kutazama zaidi.