Jumatatu , 21st Sep , 2020

Pep Giardiola leo usiku ataiongoza timu ya Manchester City kwa msimu watano, akiwa kocha wa mabingwa hao wa zamani wa EPL kwa misimu miwili mfululizo.

Pep Guardiola ameshindwa kushinda ubingwa wa klabu bingwa ulaya licha ya kutumia pesa nyingi kwenye usajili

Kocha huyo raia wa Hispania mwenye umri wa miaka 49 alijiunga na City mwaka 2016 baada ya kuondoka Bayern Munich ya Ujerumani.

The Citizens watakabiliana na Wolves inayonolewa na kocha Nuno Espirito Santos, Mbweha hao huwa wagumu sana kufungika hasa wanapocheza kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Molineux.

Nuno amempoteza mmoja ya wachezaji wake bora Diego Jota aliyejiunga na Liverpool katika dirisha hili la majira ya joto, vilevile ameondokewa na Matty Doherty aliyetimkia Tottenham Hotspurs

Licha ya kuondokewa na nyota hao,bado timu hiyo inawachezaji ambao wanauwezo wa kufanya vizuri wakiwemo Raul Gimenez, Leandor Dendoker, Ruben Neves na Joao Motinho.

Guardiola, ameshinda makombe yote ya ndani nchini Uingereza EPL mara 2,FA mara moja na kombe la ligi mara 2.

Msimu huu unategemewa kua ni mgumu sana kutokana na timu nyingi kujiimarisha kwa kufanya usajili mkubwa sana.

Liverpool,Chelsea,Arsenal,Manchester United na Tottenham zote zimejiimarisha kwa kiasi kikubwa sana.

Sheikh Mansoor ambaye ni mmliki wa Man City kiu yake si kushinda EPL bali ni taji la ligi ya mabingwa barani ulaya.

Mkataba wa Pep na klabu yake unamalizika mwishoni mwa msimu wa 2021 mwezi wa sita tarehe 30, mpaka sasa hakuna taarifa ya mazungumzo ya mkataba mpya baina ya pande hizo mbili.

Wasiwasi umeanza kuzuka kwa wanaofatilia taarifa za mkataba mpya kwa kocha huyo muumini wa tiki-taka, wakihofu inawezekana ikawa ni msimu wake wa mwisho wa kuwafundisha mabingwa hao wa kombe la ligi msimu uliopita nchini Uingereza.

Taarifa kutoka nchini Uingereza zinasema kushindwa kwa Pep kushinda taji la klabu bingwa ndicho kinachofanya mchakato wa majadiliano ya mkataba kuchelewa.

Guardiola, ndiye ndiye kocha aliyetumia pesa nyingi kwenye usajili tangu timu ya Manchester City iwe chini ya umiliki wa Sheikh Mansoor lakini ameshindwa kuipa klabu hiyo ubingwa wa ulaya.

KIASI CHA PESA ALICHOTUMIA PEP KUFANYA USAJILI NDANI YA MANCHESTER CITY.

MAJIRA YA JOTO 2016:

Euro-181,500,000mil

MAJIRA YA BARIDI 2017:

Euro-32,000,000mil

MAJIRA YA JOTO 2017:

Euro-219,000,000mil

MAJIRA YA BARIDI 2018:

Euro-69,000,000mil

MAJIRA YA JOTO 2018:

Euro-71,190,000

MAJIRA YA JOTO 2019:

Euro-14,700,000mil

MAJIRA YA JOTO 2020:

Euro 70,610,715mil.

REKODI YA KLABU BINGWA ULAYA PEP GUARDIOLA AKIWA KOCHA WA MANCHESTER CITY.

MSIMU WA 2016-2017

Msimu wa kwanza Pep akiwa kocha wa Manchester City haukua msimu mzuri kwake kwani alimaliza bila kushinda kombe lolote na City iliondolewa katika hatua ya 16 ya michuano ya Ulaya na timu ya Monaco kutokea Ufaransa.

MSIMU WA 2017-2018

Msimu wa pili katika jiji la Manchester Guardiola aliiongoza The Citizens kumaliza wakiwa washindi wa makombe mawaili ambayo ni kombe la EPL sambamba na kombe la ligi nchini Uingereza.

Haukua msimu mzuri kwa mabingwa hao wa Uingereza katika klabu bingwa kwani walitolewa katika hatua ya robo fainali na timu ya Liverpool.

MSIMU WA 2018-2019

Ulikua msimu mzuri sana kwa wapinzani hao wa jadi wa Manchester United kwani walishinda makombe yote nchini Uingereza walitwaa EPL,FA,Carabao Cup pamoja na ngao ya jamii,kama ilivyo kawaida hawakua na msimu mzuri Ulaya kwani walitokewa tena katika hatua ya robo fainali na Tottenham Hotspurs.

MSIMU WA 2019-2020

City, ilimaliza msimu ikiwa mabingwa wa kombe la ligi na iliachwa kwa alama zaidi ya 20 na mabingwa Liverpool.

Kwenye mashindano ya Ulaya matajiri hao wa jiji la Manchester, hawakufanya vizuri kwenye mashindano ya Ulaya kwa ngazi ya klabu kwani walitolewa na timu ya Olympique Lyon katika hatua ya Robo fainali.

Ikumbukwe kwa mara ya mwisho Pep Guardiola ameshinda kombe la klabu bingwa barani Ulaya ilikua mwaka 2011 kipindi alipokua anaifundisha timu ya Barcelona.

Kwa matumizi aliyofanya Guardiola tangu mwaka huo mpaka sasa Manchester City, inatoa ishara kuwa iwapo kocha huyo atashindwa kushinda taji la klabu bingwa barani Ulaya itakua ni msimu wa mwisho kwa kwake kwani atakua ameshindwa kutimiza malengo ya Sheikh Mansoor .