Jumatatu , 21st Mei , 2018

Kocha Hans Van der Pluijm wa kikosi cha Singida ameuaga uongozi wa klabu yake ya Singida kwa madai ya kuwa anaondoka bila kutaja ataelekea wapi msimu ujao.

Kocha Hans ambae alijiunga na timu hiyo  mapema mara baada ya timu hiyo kupanda daraja msimu uliopita wa 2016/17 alitokea katika klabu ya Yanga.

Kulikuwa na taarifa nyingi ambazo zilikuwa zinamuhusisha kocha huyo kujiunga kwenye klabu ya Azam Fc ili kurithi mikoba Mromania Aristica Cioba ambaye ameonekana kutokutoa kile kilichotarajiwa ndani ya klabu ya azam

Yawezekana ikawa ni safari rasmi ya kuelekea Azam FC ambayo imetajwa kumsajii tayari kuchukua nafasi ya Mromania aliyeondoka na tayari kukiongoza katika maandalizi ya msimu ujao.