Jumanne , 29th Sep , 2020

Kocha wa Mikel Arteta anahisi timu yake ya Arsenal bado wako nyuma sana ya Liverpool, lakini walipata kitu cha kujifunza kwenye mchezo wa ligi kuu ya Uingereza uliopigwa jana ambapo The Gunners walinyukwa kwa bao 3-1.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta akitoa maelekezo kwa wachezaji wake.

Akiuzungumzia mchezo huo, Arteta amesema '' Ukweli ni kwamba Liverpool ni bora kuliko sisi katika nyanja nyingi. Unaweza kuona hivyo katika hatua kadhaa.

''Nina furaha sana kwa jinsi timu ilishindana na kuendelea kuamini.Hiki ndicho kiwango tunachopaswa kufikia. Tuko kwenye safari tofauti, wamekuwa pamoja miaka mitano, tumekuwa na miezi michache. Tumekuwa safari ndefu ya kufikia tunakotaka. "

Arsenal ilianza kupata bao dakika ya 25 lililofungwa na Alexander Lacazzete kabla ya Sadio Mane kusawazsisha dakika ya 28, Andrew Robertson akawaongezea mabingwa hao watetezi bao la pili dakika ya 34 huku Diogo Jota akipachika bao dakika ya 88 ya mchezo.

Naye kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp alisema"Nina furaha kabisa na uchezaji wetu. Tulicheza mpira mzuri, tulibadilika, tukachanganya.

"Nimefurahia sana kiwango cha Diogo Jota. Ni mchezaji wa kiwango cha juu. Ni ngumu sana kuboresha timu kama yetu. Amekuwa kwenye orodha yangu kwa miaka miwili au mitatu, yuko hapa sasa."

Kuhusu kuifikisha alama tisa sawa na Leicester na Everton Klopp aliongeza, Meneja wa Everton, Carlo Ancelotti alifanya biashara nzuri. Sishangai kabisa. Leicester ni Leicester,  wanacheza mpira mzuri. Je! Ni nani anayejali katika wakati huu ni nani aliye hapo juu ? Huu ni mwanzo tu. "

Liverpool imeendeleza rekodi ya  kucheza bila ya kupoteza michezo ya EPL katika uwanja wake wa nyumbani wa Anfield ambapo imecheza jumla ya michezo 61.