
Patrick Aussems kushoto na mashabiki wa Simba.
Patrick Aussems amesema mwanzo mzuri hatua ngumu ya makundi ni sababu ya nguvu kubwa ya mashabiki wa ajabu wa Simba ambao wamekuwa wakiipa nguvu Simba.
''Asante kwa msaada wa mashabiki wote wa Simba, soka safi, ushindi mnono, ulinzi imara na umiliki mzuri wa mpira hakika ni zawadi tosha kwenu mashabiki wa ajabu kabisaa wa Simba'', amesema.
Baada ya ushindi wa jana, Simba sasa inaongoza Kundi D ikiwa na alama 3 na mabao matatu, ikifuatiwa na Al Ahly yenye alama 3 na mabao mawili baada ya ushindi dhidi ya AS Vita Club ya DR Congo.
Mchezo wa pili Simba itasafiri kwenda DR Congo kucheza na Vita Club Januari 19.