Alhamisi , 9th Jul , 2020

Klabu ya Real Betis ya ligi kuu ya Hispania imemtangaza kocha Manuel Pellegrini kuwa kocha wao mkuu kwa mkataba wa miaka mitatu.

Kocha wa Real Beti Manuel Pellegrini(pichani kulia) akiwa na aliyekua nahodha wa Man City Vicent Company (pichani kushoto) wakibeba kombe la PL walioltwaa msimu wa 2013/14

Raia huyo wa Chile mwenye umri wa miaka 66, ataanza kukinoa kikosi hicho msimu ujao baada ya kutimuliwa kwa Rubi mwezi uliopita baada ya kufanya vibaya katika mechi tatu za mwazo tangu kurejea kwa ligi baada ya Covid-19.

Pellegrini alikuza wasifu wake baada ya kuiongoza klabu ya Villareal mwaka 2006 baada ya kuifikisha hadi nusu fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya, lakini akaongeza umaarufu wake kwa kuifikisha hatua ya robo fainali ya michuano ya vilabu Ulaya klabu ya Malaga mwaka 2013.

Alijiunga na Manchester City ambapo aliipa taji la ligi kuu ya England katika msimu wa 2013/14 kabla ya kutimuliwa.

Kabla ya kujiunga na Betis, alikua kocha wa klabu ya West Ham United ambayo haikufanya vizuri mikononi mwake na kutimuliwa Disemba mwaka jana.

Real Betis haipo katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi kuu ya Hispania ambapo inakamata nafasi ta 13 ikiwa na alama 41.