Jumatano , 16th Oct , 2019

Mlinzi wa kati wa Taifa Stars Erasto Nyoni, ameweka wazi kuwa kikosi chote cha taifa stars kiko salama nchini Sudan na kinajiandaa kuivaa Sudan siku ya Ijumaa.

Wa pili kutoka kulia ni Erasto Nyoni alipokuwa nahodha wa Taifa Stars kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Rwanda.

Akiongea usiku wa kumkia leo, Nyoni ameeleza kuwa baada ya kufika Sudan salama, kinachofuata ni maandalizi mazuri tu na tayari walianza na mazoezi jana jioni Oktoba 15, 2019.

'Tunamshukuru Mungu tumetoka Rwanda na kufika hapa Sudan salama, hali ya hewa sio mbaya sana hivyo tunajiandaa tu na mchezo wetu na tayari tumefanya mazoezi baada tu ya kufika hivyo watanzania watuombee, tunaimani tutashinda', amesema.

Mchezo huo wa marudiano kuwania kufuzu CHAN dhidi ya Sudan utachezwa Ijumaa Oktoba 18, 2019 kwenye uwanja wa El Merriekh mjini Omdurman. Matokeo ya mchezo wa kwanza Taifa Stars ilifungwa 1-0 kwenye uwanja wa taifa.