Jumatano , 23rd Sep , 2020

Georginio Wijnaldum amekataa kuongeza mkataba mpya katika timu ya yake ya Liverpool, kwa maana moja au nyingine atakuwa huru kuondoka baada ya msimu huu 2020/2021 kumalizika majira ya kiangazi mwakani.

Kiungo wa Liverpool, Georginio Wijnaldum kwenye moja ya mchezo wa EPL.

Wijnaldum kiungo Mholanzi  ambaye amepata mafanikio makubwa na klabu ya  Liverpool, amegoma kuongeza mkataba mpya  wa kuendelea kuwepo klabuni hapo, licha ya kuhitajika katika mipango ya kocha  Jurgen Klopp.

KWANINI ANATAKA KUONDOKA?

Wadadisi wa mambo wanaona kama  ni  njia ya kumkimbia kiungo mpya katika timu hiyo, Thiago Alcantara  aliyejiunga  kutokea Bayern Munich  katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi.

Wijnaldum amekuwa akihusishwa na kujiunga na Barcelona  tangu Mholanzi mwenzake  Ronald Koeman achukue jukumu la kuifundisha timu hiyo.

Ujio wa Thiago  Alcantara  umezua hofu kwa baadhi ya wachezaji wa  liverpool, kutokana na umahri wake wa kuchezesha timu, kupiga pasi za uhakika, ubunifu wa hali ya juu na usahihi wa matendo yake mchezoni, ukifananisha  na viungo wengine wote wa liverpool akiwemo   Wijnaldum

Wijnaldum ambaye amecheza  michezo 189 tangu ajiunge na   klabu hiyo mwaka  2016 akitokea  Newcastle ambapo ameshiriki ipasavyo katika mafanikio ya liverpool kwenye kutwaa ubingwa  wa ligi ya mabingwa Ulaya, ubingwa wa ligi kuu England  na ubingwa wa  kombe la Dunia la  FIFA kwa ngazi ya vilabu 2019