Ligi ya Tanzania yajihakikishia wawili AFCON

Jumatatu , 10th Jun , 2019

Timu mbalimbali za taifa zilizofuzu michuano ya AFCON 2019 nchini Misri, zimeendelea kutaja vikosi vyake huku Zimbabwe ikiwa ni moja ya nchi zilitangaza wachezaji wake kamili 23 watakipiga huko na miongoni mwao wawili wanatoka TPL.

Thabaan Kamusoko

Zimbabwe imewataja Kiungo wa Yanga Thabaan Kamusoko na mshambuliaji wa Azam FC Tafadzwa Kutinyu, katika kikosi hicho cha wachezaji 23.

Kamusoko ambaye msimu huu amecheza vizuri akiwa na Yanga, amekuwa kwenye kiwango bora licha ya kumaliza msimu wa 2017/18 akiwa majeruhi. Kutinyu yeye pia amekuwa na wakati mzuri tangu alipojiunga na Azam FC msimu wa 2018/19 akitokea Singida United.

Pia kuna wachezaji mbalimbali kutoka klabu za Afrika Kusini, ikiwemo Baroka FC anayochezea mlinzi Abdi Banda wa Tanzania. Mchezaji kutoka Baroka FC ni Elvis Chipezeze.

AFCON 2019 itaanza Ijumaa Juni 21, 2019  na kumalizika Julai 19, 2019.