Jumatano , 30th Sep , 2020

Beki wa zamani wa Manchester United Gary Neville ameitaka klabu yake hiyo ya zamani ifanye maboresho zaidi kwa kusajili wachezaji watatu kabla ya dirisha la usajili halijafungwa Oktoba 05.

Gary Neville ameshinda mataji 20 akiwa na kikosi cha Manchester United kati ya mwaka 1992 mpaka 2011

Man United ni miongoni mwa timu ambazo hazijafanya usajili mkubwa miongoni mwa timu za ligi kuu England EPL, kwani mpaka sasa wamemsajili mchezaji mmoja tu kiungo raia wa Uholanzi Donny Van de Beek kutoka Ajax kwa ada ya uhamisho ya pauni million 35 ambayo ni zaidi ya ya Bilion 104 kwa fedha za kitanzania.

Timu wanazo shindana nazo kuwania ubingwa na nafasi nne za juu, Chelsea, Liverpool, Manchester City na hata Tottenham zote zimeboresha vikosi vyao kwa kusajili wachezaji wapya.

Gary Neville ambae kwa sasa ni mchambuzi ameandika kupitia ukurasa wake wa twita

“Inashangaza, hili ni moja kati ya dirisha la usajili jepesi kwenye historia ya premier League kufanya usajili lakini United hawajafanya chochote, lazima wampatie Ole beki wa kati, beki wa kushoto na mshambuliaji kabla ya dirisha kufungwa”

Maneno ya Neville yanafuatia kutokana na kikosi cha Manchester United kuonyesha kiwango kisicho cha kuridhisha katika michezo miwili ya ligi kuanzia kwenye mchezo wa kwanza ambao walipoteza dhidi ya Crytal Palace kwa mabao 3-1 lakini hata kwenye mchezo dhidi ya Brighton ambao walishinda kwa mabao 3-2 licha ya ushindi huo lakini timu haikucheza vizuri.

Wachezaji kadhaa wamekuwa wakihusishwa kujiunga na Manchester United kabla ya dirisha la usajili kufunga wachezaji kama Harry Kane, Alex Telles, Ousmane Dembele, Edinson Cavani na Luka Jovic.

Gary Neville aliitumikia Manchester United kwa misimu 19 toka mwaka 1992 mpaka 2011 na alishinda jumla ya mataji 20, ukiwemo ubingwa wa ligi kuu England EPL mara 8 na ubingwa wa klabu bingwa ulaya mara 2.

Msimu uliopita Yanga ilifunga mabao 45 kwenye michezo 38 ya liki kuu ambao ni wastani wa bao 1.18 kwa mchezo.

Msimu huu katika michezo 4 ya ligi timu ya wananchi imefunga mabao