Manara amvaa Kindoki, mwenyewe ampa majibu haya

Jumapili , 15th Sep , 2019

Msemaji wa Klabu ya Simba Haji Manara ameonekana akitupiana maneno na Mjumbe wa Kamati ya Hamasa wa Yanga, Jimmy Kindoki, ikiwa ni siku chache baada ya kumalizika kwa sare ya 1-1 katika mchezo wa kuwania makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, dhidi ya Zesco United uliochezwa jana.

Maneno hayo yalianza kwa Haji Manara aliyepost video fupi katika mtandao wa Instagram ikimuonyesha Jimmy Kindoki huku ameandika kuwa

Nimesikitika sana mtu anayetambulika eti Mjumbe Kamati ya Hamasa ya Yanga kuwataka wafuasi wao wa-deal na washabiki wa Simba walioenda taifa jana, hii ni fedheha kwa mchezo wa mpira na aibu kwa klabu yake iliyompa 'dhamana' hewa, naomba tena na tena vitu hivi vya hovyo hovyo tuviache, laa sivyo soka tutaiharibu ladha yake” aamemandika Haji Manara

Akijibu madai hayo Jimmy Kindoki ameandika kuwaz “we mzee nakuheshimu ila unapoelekea sasa naona ni personal, hakuna sehemu niliyosema mashabiki wa Simba wapigwe wala hakuna video inaonesha nikimpiga mtu pale uwanjani, mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Hamasa na si bondia"

Aidha Kindoki amedai kuwa Kazi yake ni kuhakikisha watu wanakuja uwanjani na hata wakienda washangilie mwanzo mwisho, asitake kuaminisha watu waliopigwa yeye ndiyo nimesababisha na hataki kugombana na watu wa Mashabikiwa Simba.