Jumatano , 23rd Sep , 2020

Mkuu wa Idara ya habari na mawasiliano wa Simba Haji Manara amewaomba mashabiki kuwa na utamaduni wa kununua tiketi ambazo za kisasa mapema kuliko kukimbilia siku ya mechi ili kuepeuka usumbufu pale wanapohitaji kuingia kutazama mchezo.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara akizungumza na waandishi wa habari.

Manara amesema wamejaribu kuongea na wasimamizi wa mauzo ya tiketi katika viwanja vya Mkapa na uhuru kuwa na utaratibu rafiki ambao hautawakwaza mashabiki wao ambao wamekuwa wakiitikia wito wa kuja uwanjani kuangalia mpira.
 

''Tuwaombe mashabiki wetu waanze kuwa na ule utamaduni wa kununua hizi tiketi ambazo ni za kisasa,mapema zaidi kuliko kusubiria siku ya mechi.

.Changamoto kubwa ni kwamba tunao baadhi ya watu wao hupenda kununua tiketi siku ya mchezo wenyewe, hii hupeleka kuwepo na msongamano usio na ulazima''

Simba Sc itajitupa dimbani Septemba 26 mwaka huu kiwakabili wageni wa VPL Gwambina fc katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Daresalaam majira ya Saa 1:00 usiku.