Jumatatu , 9th Mar , 2020

Klabu ya Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi dhidi ya Simba kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka minne iliyopita.

Haji Manara na Patrick Aussems

Mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Taifa, ilishuhudiwa Yanga ikiwazuia Simba kwa ushindi mwembamba wa bao moja kwa sifuri.

Kufuatia matokeo hayo, Afisa Habari wa Simba, Haji Manara ambaye hakuwepo nchini jana wakati wa mchezo, amewaomba mashabiki wa klabu hiyo kutulia na kuungana kwa ajili ya mechi zilizobakia.

Kwa upande wake, aliyewahi kuwa kocha wa klabu hiyo, Patrick Aussems amesema kuwa amesikitishwa na matokeo hayo, lakini akisema kuwa alitarajia kwa hicho kilichotokea.