Manusura wa ajali arejea uwanjani

Thursday , 14th Sep , 2017

Mchezaji wa klabu ya soka ya Chapacoense ya Brazil Alan Ruschel ambaye alinusurika kwenye ajali ya ndege mwaka jana amecheza mechi yake ya kwanza ya ushindani usiku wa kuamkia leo.

Alan alipona pamoja na wenzake wawili ambao ni Neto na Jackson Follman huku abiria wengine 71 wakipoteza maisha katika ajali hiyo. 

Mlinzi huyo wa kati amecheza dakika 73 katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya makundi katika ligi ya mabingwa Amerika Kusini dhidi ya Flamengo ambapo timu hizo zimetoka sare tasa.

Ruschel amekuwa akitokwa na machozi mara zote anapoingia uwanjani ambapo mara ya kwanza alicheza dakika chache kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Barcelona. Flamengo na Chapacoense zitarejeana tena Septemba 20 mwaka huu.