Alhamisi , 13th Aug , 2020

Kocha mkuu wa timu ya Real Madrid Zinedine zidane amesema hata sajili mchezaji yeyote katika dirisha hili kubwa la usajili baada ya kuridhika na timu yake iliyotwaa ubingwa wa la liga msimu huu, Pamoja na kutolewa katika ligi ya mabingwa Ulaya

Martin Odegaard akiwa na timu ya Real Sociadad katika mechi ya la liga dhidi ya Real Madrid

Wameamua kumrudisha mchezaji wao raia wa Norway Martin  Odegaard aliyekuwa anacheza Real Sociedad kwa mkopo, Martin mwenye umri wa miaka 21 pamoja na kusajiliwa akiwa kinda  amekuwa akitolewa kwa mkopo wa muda mrefu

Odegaard alisajiliwa na Real  Madrid  akiwa kinda wa umri wa miaka 16  kutoka nyumbani  kwao Norway na  wengi waliamini  kipaji chake ni cha  juu hadi kufananishwa na akina  Messi na  Cristiano Ronaldo lakini haikuwa hiyo

Msimu huu akiwa na Real Sociedad   amefanya vyema kwa kutoa mchango mkubwa  wa moja kwa moja hadi kupelekea Zidane   kumrejesha tena katika kikosi.