Masau Bwire amtia mkwara Morrison wa Yanga

Jumamosi , 8th Feb , 2020

Kuelekea mchezo wa leo wa ligi kuu soka Tanzania bara kati ya Yanga dhidi ya Ruvu Shooting, msemaji wa Ruvu Masau Bwire ameweka wazi kuwa hawatamvulimia Morrison kwa vitendo vyake vya kutembea juu ya mpira.

Masau Bwire na Bernard Morrison

'Ukiangangalia kikosi cha Yanga hakina maajabu, hakuna mchezaji ambaye sisi hatuna, kwahiyo Papasa Squared iko palepale kama tulivyofanya mzunguko wa kwanza', amesema Masao.

Akimwongelea mchezaji wa Yanga aliyesajiliwa wakati wa dirisha dogo Bernard Morrison, Masau amesema, 'Hizo Mbwewe zake za kutembea juu ya mpira alikuwa anafanya kwa timu ambazo hazina watu, kwetu hatofanya na kama atajaribu hatavumilika'.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa leo Saa 10:00 kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam. Katika mchezo wa kwanza Ruvu Shootinga walishinda goli 1-0.

Yanga kwasasa ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 34 kwenye mechi 17, huku Ruvu Shooting ikiwa nafasi ya tisa ikiwa na pointi 26 kwenye mechi 19.