Ijumaa , 24th Mei , 2019

Klabu ya soka ya Simba, imetoa utaratibu wa jinsi mashabiki wake watashangilia kombe lao kesho Mei 25, 2019, baada ya kukabidhiwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Mashabiki wa Simba mkoani Singida wakishangilia

Akiongea leo Mei 24, 2019, msemaji wa timu hiyo Haji Manara, amesema mashabiki wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo dhidi ya Biashara Mara utakaoanza majira ya saa 9:00 mchana kwani kiingilio kimepunguzwa.

''Tumepunguza kiingilio kutoka 5000/= hadi 3000/= ili mashabiki wote waje kushuhudia timu yao ikikabidhiwa kombe la ubingwa wa ligi kuu msimu wa 2018/19'', amesema.

Aidha Manara amebainisha kuwa kwa kuzingatia huu ni mwezi mtukufu na mashabiki wa Simba ambao wamefunga ndio maana wakaomba mchezo huo uanze mapema ili wawahi kurudi na kufuturu.

Zaidi kuhusu barabara watakazopita kwenye basi maalumu wakiwa na kombe lao, msikilize Manara hapo chini akifafanua.