Ijumaa , 17th Sep , 2021

Mashabiki wa Manchester City wamemjia juu Kocha mkuu wa timu yao, Pep Guardialo baada ya kutoa kauli ya kuwahimiza wajitotekeze kwa wingi kwenye dimba la Etihad siku ya Jumamosi dhidi ya Southampton.

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola (chini kulia) aliyewashukia mashabiki kuwataka wajitokeze uwanjani kwa nguvu wakati Manchester City itakapocheza na Southampton saa 11:00 jioni.

Guardiola alieleza masikitiko yake juu ya uchache wa mashabiki katika mchezo ligi ya mabingwa barani Ulaya, kwenye ushindi wa 6-3 dhidi ya RB Leipizg  ambapo mashabiki 38,000 waliingia uwanjani kati ya viti 55,000 vilivyopo.

Mashabiki wa City kupitia, katibu mkuu wa kilabu rasmi cha wafuasi wa Mabingwa hao wa Uingereza, Kevin Parker anataka Guardiola azingatie zaidi mazingira, akisisitiza Mhispania huyo haelewi shida ambazo mashabiki wanakabiliwa nazo.

"Sina hakika kama anaelewa mambo jinsi yalivyo, Haelewi ugumu ambao watu wengine walipitia kufika Etihad siku ya Jumatano.'' kitendo hicho Kilimshangaza sana, Parker amesema.

"Wana watoto wa kufikiria, wanaweza wasiweze kumudu, bado kuna maswala kadhaa kuhusu UVIKO-19 . Sioni ni sababu kilichomsukuma kuzungumzia jambo hili'' Alisema Parker.