Ijumaa , 10th Jul , 2020

Kuelekea mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Jumapili hii kati ya Simba na Yanga, mashabiki na wanachama wa timu hizo mkoani Ruvuma wameanza kutunishiana misuli juu ya uwezo wao.

Mshabiki wa Simba na Yanga

Licha ya kuchukua ubingwa wa ligi kuu mapema, mashabiki wa Simba wanasema msimu huu ni mwendo wa vikombe vyote na yale ya tarehe nane hayatajirudia tena kwani wana kikosi kipana sio kama watani wao ambao wamempigia magoti Morisson. 

Nao mashabiki wa Yanga wamejibu wakisema kuwa katika historia yao, hawajawahi kufungwa na Simba siku ya Jumapili. Pia hawajawahi kupoteza mechi dhidi ya Simba kwenye mwaka unaogawanyika kwa mbili.

Watazame hapa wakijinadi.