Jumapili , 10th Feb , 2019

Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri amesema kushuka kwa uzalishaji mali kwa wananchi wilayani humo hivi sasa kunasababishwa na matukio ya utekaji na mauji ya watoto yanayoendelea.

Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri

Amesema hali hiyo inatokea kwa kuwa wazazi wanatumia muda mwingi kwapeleka watoto na kuwafuata watoto shule hivyo kupoteza muda na kusimamisha shuguli zao.

Ameyasema hayo jana, Februari 9 wakati akifunga maombi katika  Kanisa la TAG Milinze yaliyolenga kuombea Wilaya hiyo.

Hatuwezi kufikia uchumi wa Viwanda kama matukio haya yataendelea wazazi wanapoteza sana muda katika kuhakikisha watoto wao wanapata ulinzi kwa kuwapeleka na kuwarudisha nyumbani”, amesema Ruth Msafiri.

Niwaambie tu Halmasahuri ya Mji wa Njombe inaoongoza katika Halmashauri zote nchini kwa kuwa na kipato kikubwa kwa mwaka, mwananchi wa hapa ana uwezo wa kuwa na shillinhi million 5” ameongeza.

Pia Mkuu huyo wa Wilaya amewataka waumini wa Kanisa hilo na wananchi wa Wilaya na Mkoa wa Njombe kwa ujumla kuombea mkoa wao ili kuondokana na vitendo hivyo vinavyopelekea kuzorotesha shughuli za kiuchumi.

Akitoa salama za Wizara Mwenyekiti wa Timu ya Wataalam kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ( Idara za Maendeleo na Ustawi wa Jamii) Bi. Hanifa Selengu amesema Serikali ipo pamoja na wananchi wa Mkoa wa Njombe katika kulaani matukio hayo ya utekeaji na mauaji ya watoto yaliyojitokeza.