Alhamisi , 17th Jun , 2021

Aliyekuwa mgombea urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Ally Mayay amesema hatakata rufaa baada ya kuenguliwa kwenye kinyan'ganyiro hicho.

Ally Mayay Tembele9( kulia) akizungumza na aliyekuwa kocha wa Yanga Hans Van Pluijm

Mayay alienguliwa jana baada ya kushindwa kukidhi baadhi ya vigezo vya kikanuni kama kukosa uthibitisho wa wadhamini (endorsement) kutoka kwa wajumbe watano.

"Mimi ni mwanafamilia wa michezo na napenda kuona maendeleo na ninaweza kusaidia hata kama nisipokuwa Rais wa TFF, naweza kuisaidia maendeleo ya soka hata nikiwa katika nafasi niliyopo. Sifikirii kukata rufaa," amesema Mayay.

Katika uchaguzi uliofanyika Agosti 12, mwaka 2017 kwenye ukumbi wa mikutano wa jengo la St. Gasper Jijini Dodoma, Mayay aligombea nafasi na akashindwa na Karia aliyekuwa anagombea kwa mara ya kwanza Urais wa TFF.

Karia alipata kura 95 kati ya 125 zilizopigwa, akifuatiwa na Ally Mayay aliyepata  9 sawa na mgombea mwingine, Shija Richard waliopata kura 9 kila mmoja.