Jumatatu , 11th Sep , 2017

Kocha Mkuu wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Young Africans, George Lwandamina amefunguka na kudai walilazimika kubadili mbinu za mchezo kutokana na hali ya mazingira kuwa tofauti na wao walivyozoea.

Kocha Mkuu wa Yanga mwenye uraia wa Zambia, George Lwandamina.

Lwandamina ameeleza hayo asubuhi ya leo kupitia ukurasa wao maalum wa klabu baada ya timu yake kutoka kifua mbele siku ya jana (Jumapili) kwa kuwachakaza Njombe Mji FC kwa bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji Ibrahim Ajib kwa kutumia mkwaju wa adhabu.

"Tulijua utakuwa mchezo mgumu, kipindi cha pili tulilazimika kubadili mbinu ili kukabiliana na mazingira. Nawashukuru wachezaji hakika walifanya kazi kubwa dakika zote 90 za mchezo", amesema Lwandamina.

Kwa upande mwingine, timu ya Mtibwa Sugar kwa sasa ndiyo ambayo inaongoza ligi kwa mujibu wa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa pointi sita, akifuatiwa na Simba SC kwa pointi nne, Tanzania Prisons alama nne.