Mbeya City yammwaga Mmalawi Kinnah Phiri

Wednesday , 13th Sep , 2017

Klabu ya ligi kuu soka Tanzania Mbeya City, leo Septemba 13, 2017 imeachana na kocha wake mkuu Mmalawi Kinnah Phiri ambaye ameitumikia klabu hiyo kwa msimu mmoja.

Kocha wa Mbeya City Kinnah Phiri

Mbeya City imethibitisha hilo kupitia kwa Katibu Mkuu wake Emmanuel Kimbe. "Ni kweli tumeachana na Phiri kwasababu za kimasilahi ikiwemo madai yake ya kulipwa mshahara mkubwa", amesema Kimbe.

Mbeya City sasa itaendelea na kocha wake Mohammed Kijuso ambaye amechukua mikoba ya Phiri na kuiongoza timu hiyo katika michezo miwili ya ligi kuu ya soka Tanzania bara.