Mbio za magari duniani ni zamu ya Singapore

Wednesday , 13th Sep , 2017

Mbio za magari kuwania ubingwa wa dunia msimu wa 2017 zinatarajiwa kuendelea Septemba 17 nchini Singapore ikiwa ni raundi ya 14 baada ya kupita katika miji mbalimbali duniani.

Mbio hizo zitafanyika usiku wa Ijumaa kwenye mitaa ya Marina Bay huko Singapore ambapo mitaa hiyo inafahamika kwa kuwa na barabara zenye kona nyingi na mara nyingi mshindi wa mbio hizo huibuka bingwa wa dunia.

Kuelekea mbio hizo, dereva wa timu ya Mercedes, Muingereza Lewis Hamiliton anaongoza msimamo akiwa na alama 238, akifuatiwa kwa karibu na Sebastian Vettel wa Ferrari mwenye alama 235.

Vartteri Bottas kutoka Mercedes anashika nafasi ya tatu akiwa na alama 197. Katika mbio za Singapore Grand Prix Mjerumani Sebastian Vettel anarekodi nzuri zaidi ya kushinda akiwa ameshinda mara 4 huku mpinzani wake mkubwa Lewis Hamiliton akiwa ameshinda mara 2.