Jumamosi , 20th Apr , 2019

Taarifa iliyoripotiwa na mtandao wa sportinglife.ng n inasema kwamba taifa la Guinea limempoteza mwanasoka chipukizi Aly Soumah, ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha Guinea U-17 kilichokuja Tanzania kwa ajili ya michezo ya AFCON U-17.

Aly Soumah ambaye alirudishwa kwao baada ya kugundulika kuwa alidanganya kwenye taarifa zake na kutokidhi vigezo vya kuwa kwenye kikosi hiko, alipata ajali ya gari katika eneo la Kindia nchini kwao Guine na baadae kufariki.

Mchezaji kudanganya umri

 

Kutokana na kipimo  cha MRI kuonesha kuwa Aly kavuka umri, alilazimika kurudishwa kwao kabla ya mchezo wa ufunguzi wa AFCON kati ya timu yake ya Taifa ya Guinea katika uwanja wa Chamazi Dar es Salaam dhidi ya Cameroon ambapo katika mchezo huo Cameroon walishinda 2-0.

Mchezaji Aly Soumah