Jumamosi , 24th Mar , 2018

Kiungo wa timu ya taifa ya Hispania David Silva ataukosa mchezo wa kirafiki kati ya timu hiyo dhidi ya Argentina baada ya kuondolewa kambini kwa sababu iliyoelezwa kuwa ni masuala binafsi.

Silva alijumuishwa kikosini na kocha Julen Lopetegui na jana usiku alicheza dakika 71, kwenye mchezo wa kirafiki ambapo Hispania ilitoka sare ya bao 1-1 na Ujerumani lakini kocha huyo amelazimika kumhuruhusu nyota huyo akashughulikie mambo yake.

Mchezo wa kirafiki wa Hispania na Argentina utapigwa siku ya Jumanne Machi 27, kwenye uwanja wa Wanda Metropolitano unaomilikiwa na klabu ya Atletico Madrid inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa La Liga.

Hivi karibuni pia kocha wa Manchester City Pep Guardiola alilazimika kumpa mapumziko Silva baada ya mtoto wake anayefahamika kama Mateo kuzaliwa akiwa na siku pungufu hivyo muda mwingi akawa anahitajika kuwa karibu na familia yake.

Klabu yake hiyo ambayo inaaongoza ligi kuu ya England itarejea dimbani Machi 31 kuivaa timu ya Everton kwenye mwendelezo wa michezo ya  ligi kuu ikiwa katika hatua za lala salama kw amsimu wa 2018/19.