Mchezaji wa kimataifa wa Simba arudi kwao

Jumatatu , 7th Oct , 2019

Kiungo wa kimataifa wa Kenya anayekipiga katika klabu ya soka ya Simba, Francis Kahata, amerejea nchini kwao kwa ruhusu maalumu ya kumuuguza mtoto wake.

Francis Kahata

Kahata ambaye ameseajiliwa na Simba msimu huu, ameileza EATV & EA Radio Digital, kuwa mtoto wake wa kike anasumbuliwa na figo.

'Nipo Kenya nimekuja kumuuguza mtoto wangu, anaumwa figo na amelazwa katika hospitali moja huku ila anaendelea vizuri', - amesema Kahata.

Mtoto wa Kahata akiwa hospitali na daktari.

Tangu kusajiliwa kwake ndani ya klabu ya Simba, Kahata amecheza mechi kadhaa zikiwemo mbili za Ligi ya Mabingwa hatua ya awali ambapo Simba ilitolewa na UD Songo ya Msumbuji.

Hata hivyo katika kuelekea mechi za kimataifa za kalenda ya FIFA, Kahata hajaitwa kwenye kikosi cha Harambee Stars na amesema anaweza kurejea nchini kesho Oktoba 8, 2019.