Mkurugenzi aungana na Mo Dewji Simba

Jumanne , 25th Jun , 2019

Aliyekuwa mkurugenzi wa ufundi wa shirikisho la soka nchini, Ammy Ninje, amesema mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu za Tanzania unahitajika ili soka letu lipige hatua.

Mohammed Dewji

Akiongea katika mahojiano na 5SPORTS ya East Africa Television, Ammy Ninje ameeleza kuwa kama serikali tayari imeshaweka utaratibu mzuri wa mgawanyo wa hisa kwa mwekezaji na wanachama hivyo ni vizuri ukafuatwa.

''Tunahitaji kubadilika ila tusikurupuke, tuwape timu wawekezaji ili tuone baada ya muda kama tutapiga hatua, kwa mfano Simba tayari wapo huko na mwekezaji ana asilimia 49, tumpe nafasi ya kufanya mabadiliko ili mwisho wa siku tuone tutafika wapi''.

Ammy Ninje ameongeza kuwa hata vilabu vikubwa vilivyofanikiwa barani Ulaya ni vya wanachama lakini vilihama kutoka kwenye mfumo huo na kwenda kwenye uwekezaji na ndio maana vina nguvu uwanjani na kiuchumi kiujumla.