Jumanne , 12th Feb , 2019

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Klabu ya Simba, Mohamed Dewji, 'Mo' amesema kwamba simba ina uwezo wa kumpiga Al Ahly siku ya leo katika uwanja wa Taifa jiijini Dar es salaam.

Mohamed Dewji

Mo ameyasema hayo yakiwa yamebaki masaa machache kuelekea mchezo dhidi ya mabingwa mara 8 wa michuano hiyo, Al Ahly.

Katika ukurasa wake wa Twitter, MO amesema kwamba, "Uwezo wa kumpiga tunao, sababu ya kumpiga tunayo, na nia ya kumpiga tunayo." Tukutane Taifa! Uzalendo Kwanza! #YesWeCan".

Katika mchezo uliopita, Simba ilichezea kipigo cha goli 5-0 katika uwanja wa Borg el Arab mjini Alexandria, nchini Misri, ikiwa ni kichapo cha pili baada ya kile cha AS Vita Club.

Simba ipo nafasi ya tatu katika kundi 'D' kwa pointi tatu huku Al Ahly ikiongoza kundi kwa pointi 7. Nafasi ya pili inashikiliwa na AS Vita Club kwa pointi zake nne na JS Saoura ikiburuza mkia.