Mo awashikia bango mashabiki wa Simba

Alhamisi , 14th Mar , 2019

Wakati Simba ikijiandaa na mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi Klabu Bingwa Afrika wikiendi hii, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo, Mohamed Dewji 'Mo' amezidi kuwajaza mashabiki ili kuisapoti timu yao.

Mo Dewji pamoja na mashabiki wa Simba wakiwa uwanjani

Mchezo huo kati ya Simba na AS Vita Club ya DR Congo unatarajia kupigwa Februari 16 katika Uwanja wa Taifa majira ya saa 1:00 usiku ikiwa ni wiki moja baada ya kutoka kufungwa mabao 2-0 dhidi ya JS Saoura nchini Algeria.

Katika ukurasa wake wa Instagram, Mo ameweka video iliyoambatana na ujumbe unaowataka mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao huku akisisitiza kuwa naye ataungana nao uwanjani.

 

Katika msimamo wa kundi lake, Simba inakamata nafasi ya mwisho ikiwa na pointi 6 baada ya michezo mitano mpaka sasa. Nafasi ya kwanza ikishikiliwa na JS Saoura yenye pointi 8 huku Al Ahly na AS Vita Club zikiwa katika nafasi ya pili na ya tatu.

Mchezo wa Klabu Bingwa Afrika kati ya Simba na JS Saoura

Kwa nafasi ilivyo sasa, kila timu inayo nafasi ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo endapo itafanikiwa kupata ushindi katika mchezo wake wikiendi hii. Ukiachana na mchezo wa Simba na AS Vita Club, pia mchezo mwingine utapigwa nchini Misri ambapo Al Ahly itapambana na JS Saoura kutafuta nafasi hiyo.

Bonyeza hapa chini kutazama zaidi.