Jumamosi , 8th Aug , 2020

Klabu ya soka ya Simba ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara msimu wa 2019/20 imemsajili aliyekuwa mchezaji klabu ya Yanga Bernard Morrison.

Bernard Morrison akisaini mkataba Simba

Kupitia kurasa rasmi za Simba Sports Club kwenye mitandao ya kijamii mchana wa leo Agosti 8, 2020 wameweka picha za Morrison akisaini pamoja na ujumbe mfupi 'Morrison is Red'.

Morrison ambaye ni raia wa Ghana anakumbukwa kwa kuifunga Simba goli pekee lililoipa ushindi Yanga kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu soka Tanzania bara Machi 8, ambapo Yanga ilishinda 1-0.