Jumanne , 16th Oct , 2018

Huenda usilifahamu kabisa jina la mshambuliaji, Krzysztof Piatek ambaye hivi sasa anavitesa vilabu vingi barani Ulaya kutokana na uwezo wake wa kufumania nyavu katika klabu yake.

Krzystof Piatek

Mshambuliaji huyo raia wa Poland anachezea katika klabu ya Genoa inayoshiriki ligi kuu ya nchini Italia ‘Serie A’. Mpaka sasa ameshafunga mabao 13 katika mashindano yote ndani ya klabu yake msmu huu na kuwawashia taa ya kijani nyota wa dunia Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.

Piatek (23) mpaka sasa anaongoza katika listi ya wafungaji bora wa ligi mbalimbali barani Ulaya hasa ligi kubwa tano za bara hilo, akiwa ameshafunga mabao 9 akifuatiwa na Kylian Mbappe wa PSG  pamoja na Cristian Stuani wa Girona.

Kutokana na uwezo anaouonesha mpaka sasa katika ligi kuu nchini Italia, timu kadhaa barani Ulaya tayari zimeshaonesha nia ya wazi ya kutaka kumsajili mchezaji huyo ikiwemo, Fc Barcelona, Borusia Dortmund, Bayern Munich na Chelsea.

Msimu uliopita nyota wa Barcelona Lionel Messi na wa Juventus, Cristiano Ronaldo walipewa upinzani mkali katika kuwania kiatu cha dhahabu cha ufungaji bora wa ligi za ulaya na Mohamed Salah wa Liverpool, mbio ambazo Lionel Messi alishinda kwa mabao yake 34.