Mtendaji mkuu wa Liverpool ang'atuka

Ijumaa , 31st Jul , 2020

Mtendaji mkuu wa klabu ya Liverpool, Peter Moore ametangaza kung'atuka katika nafasi yake baada ya kudumu na mabingwa hao wa ligi kuu ya England kwa miaka mitatu.

Peter More (Kulia) akiwa na nahodha wa Liverpool Virgil Van Dijk (kushoto) katika picha ya pamoja wakisherekea ubingwa.

 

Nafasi ya Moore itachukuliwa na Billy Hogan ambaye ndiye mkurugenzi mtendaji na ofisa wa idara ya masoko ya klabu hiyo.

Moore anaondoka Anfield akiwa ameifanikishia Liverpool kutwaa taji lake la kwanza la EPL baada ya miaka 30,lakini akiisaidia kutwaa taji la ligi ya mabingwa Ulaya pamoja na ubingwa wa vilabu wa Dunia.

Kiongozi huyo alijiunga na Liverpool mwaka 2017 akitokea nchini Marekani ambako aliishi kwa miaka 30 alifanya kazi na kampuni mbali mbali ikiwemo Sega inayojihusisha na teknolojia ya filamu,Microsofti na ile inayojihusisha na vifaa vya michezo ya Reebok.