Mungu ajibu maombi ya mashabiki Simba na Yanga.

Sunday , 8th Jan , 2017

Maombi ya mashabiki wa Simba na Yanga visiwani Zanzibar yamejibiwa baada ya Mungu kuzikutanisha timu hizo katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi.

Hiyo ni baada ya leo Simba kuichapa Jang'ombe Boys mabao 2-0 katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi.

Katika mchezo huo Simba imeendelea kuonyesha mchezo mzuri na udhaifu wa kupata mabao licha ya kutengeneza nafasi lukuki.

Laudit Mavugo ametuma Salam kwa Yanga baada ya leo kufunga mabao yote mawili ya Simba na kuibuka mchezaji bora wa mechi hiyo.Kwa matokeo hayo, Simba imeibuka kinara wa kundi B ikifikisha point 10 ambapo kwa mujibu wa kanuni za michuano hiyo itakutana na mshindi wa pili wa kundi A ambaye ni Yanga iliyomaliza na point 6.

Katika kuelekea siku ya Simba na Yanga Mchezaji wa Simba Jonas Mkude amesema  kwa sasa Simba wamejipanga vizuri hivyo amaanini hata Yanga wamejipanga sawa sawa na kusema hawezi kujua ni timu gani itaibuka na ushindi bali dakika tisini ndiyo zitasema mshindi ni nani kati ya Simba na Yanga siku hiyo ya Jumanne.

"Kwanza nashukuru Mungu tumemaliza salama mechi kati ya Jang'ombe Boys na kupata heshima ya goli 2. Kuhusu kuelekea siku ya Jumanne naamini kila mtu amejiandaa vyema hivyo dakika tisini ndiyo zitaamua mshindi kati ya Simba na Yanga" alisema Mkude