Jumatano , 9th Mar , 2022

Nyota wa tennis raia wa England Andy Murray ameahidi kutoa mapato yake yote ya tuzo na fedha kwa kipindi kilichobaki kwa mwaka mzima kuanzia sasa ili kuwasaidia watoto walioathiriwa na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

(Mchezaji nyota wa Tennis Andy Murray)

Mwingereza huyo anafanya kazi na Unicef kutoa vifaa vya matibabu, maendeleo na samani mbalimbali nchini ukraine, amesema hadi sasa wameshuhudia zaidi ya watu milioni mbili wakiikimbia nchi hiyo, na zaidi ya watoto milioni 7.5 wako hatarini kwa kukosa mahitaji muhimu kutoakana na machafuko hayo ya kivita yanayoendelea hadi sasa.

Mshindi huyo mara tatu wa Grand Slam, ambaye ni balozi wa Unicef nchini England, pia amesema Unicef inajitahidi kuwezesha upatikanaji wa masomo kwa watoto waliohamishwa mchini humo, pamoja na kusaidia ukarabati wa majengo ya shule zilizoharibiwa.

Na bodi zinazosimamia mchezo wa tenisi duniani zimetangaza kuchangia kiasi cha dola za kimarekani laki 7 ili kusaidia juhudi za kibinadamu nchini Ukraine na kuliunga mkono Shirikisho la Tenisi nchini humo linalopitia kipindi kigumu.