
Aliyekuwa kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike akiwa amebebwa na wachezaji baada ya kufuzu AFCON
Machi 23, 2019 itakumbukwa katika historia ya Tanzania kwenye anga za kimichezo, ambapo timu ya taifa 'Taifa Stars' ilifanikiwa kufuzu michuano ya AFCON kwa mara ya kwanza baada ya miaka 39 kupita ambapo iliifunga Uganda mabao 3-0 Jijini Dar es Salaam.
Mara ya mwisho kwa Taifa Stars kufuzu michuano ya AFCON kabla ya mwaka huu ni mwaka 1980, michuano ambayo ilifanyika nchini Nigeria, ambapo haikufanukiwa kufika hatua kubwa kwenye michuano hiyo.
Katika michuano yenyewe ya AFCON 2019 iliyofanyika nchini Misri, Taifa Stars iliondolewa hatua ya makundi ikiwa haijashinda mchezo wowote, ambapo ilipoteza mechi ya kwanza dhidi ya Senegal kwa kufungwa mabao 2-0 kabla ya kufungwa na Kenya mabao 3-2 na kisha kufungwa na Algeria mabao 3-0.
Fuatilia hapa matukio makubwa ya kimichezo yaliyojiri nchini mwaka 2019.