Jumanne , 18th Sep , 2018

Mwanamasumbwi Hassan Mwakinyo amekanusha taarifa za pambano lake lililotarajiwa kufanyika Ujerumani Oktoba 20, mwaka huu dhidi, ya Bondia Mjerumani Wanik Awdijan.

Mwanamasumbwi Hassan Mwakinyo.

Akiongea na www.eatv.tv Mwakinyo, (23) amesema haja saini mkataba wowote juu ya pambano hilo na hana taarifa zozote mpaka sasa, huku akidai kuwa hawezi kushiriki mchezo huo kutokana na kuto kulingana kwa viwango (rank) na bondia huyo ambaye hawezi kumuongezea nafasi yoyote kimataifa.

Mwakinyo amesema “ Mimi naomba niwaambie watu kuwa hilo pambano hakuna, sija saini mkataba ni tuhuma tu hizo, labda waniteke nikacheze nikiwa nimefungwa mikono lakini siwezi kwenda kucheza kwasababu sina taarifa nazo, na bondia huyo awezi kunipa credit yoyote ile sababu mtu mwenyewe sio wa rank yangu".

Kuhusiana na pambano dhidi ya May Weather, Mwakinyo amesema anaamini ipo siku ataweza kupambana na bondia huyo kwani anaweza kufika huko huku akiwataka Watanzania kutoa sapoti na kuacha kasumba ya kwamba May Weather anaweza kumpiga kila mtu.

Aidha Mwakinyo amesema mpaka sasa ana Promota mmoja tu ambaye ana haki ya kuzungumzia mapambano yake na ndiye aliyemtafutua pambano lake la uingereza ambaye ni Sheikh Ali Mwazoa, huku akikiri kuendelea na Mkalimani wake.

Pia amesema hawezi kuhamisha makazi yake kutoka Tanga na kuhamia Dar es salaam kutokana na uwepo wa ndugu na marafiki zake waliopo mkoani huko kwani hana nia ya kutengeneza marafiki wapya kwa sasa.