Jumatatu , 24th Sep , 2018

Baada ya kumtwanga bondia kutoka England, Samm Eggington, Bondia Hassan Mwakinyo, ameendeleza ubabe wake wa kutaka pambano dhidi ya bondia kutoka Uingereza, Amir Khan.

Bondia Hassan Mwakinyo (kushoto) na Bondia kutoka Uingereza Amir Khan.

Akiongea na www.eatv.tv Mwakinyo amesema,hana wasiwasi na Amir khan,kwani ni bondia ambaye amekuwa akibebwa na nchi yake ngali na kuwa na kiwango hafifu na ana imani ya kuwa na uwezo wa kumchakaza bondia uyo kwa nafasi ileile aliyoitumia kwa Sam Eggington.

“_Amir khan si bondia wa kutisha anabebwa sana na watu wake, alishawahi kupigwa kwenye kidevu akapata strock (mshtuko) na kukaa nje ya mashindano kwa mwaka ,kwaiyo mimi nitampiga katika nafasi ileile ya kuumia kwake, ikiwa asilimia 5% naamini nitampiga, na 95% naomba tumuachie Mungu”_ Amesema Mwakinyo.

Akizungumzia juu ya mfadhili wake mpya ambaye pia ni Mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji, Mwakinyo amesema, anashukuru kwa sapoti anayoipata kwa sasa kupitia Mwekezaji huyo, richa ya kutokuwa na makubaliano yoyote ya kimkataba baina yao.

Taarifa hizo zimekuja mara baada ya Mwakinyo kukosa watu wa kumuwezesha kupata maandalizi ya kutosha na sasa bila shaka ndoto yake imezidi kunawili kutokana na kupata nguvu kwa Bilionea huyo kijana ndani ya Afrika.

Mwakinyo ambaye ameweka makazi yake mkoani Tanga, ameendelea kuweka mkazo kutokuwepo kwa pambano lake dhidi ya bondia wa Ujerumani Wanik Awdijan, kutokana na kuto kulingana kwa viwango (rank) akisema bondia huyo hawezi kumuongezea nafasi yoyote kimataifa.