Ijumaa , 23rd Mar , 2018

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ameeleza kupokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji wa Tanzania wa mpira wa kikapu Bi Yvvone Christopher Wambura.

Yvonne alifariki dunia Machi 21 jijini Dar es salaam ambapo kabla ya kifo alikuwa mchezaji wa timu ya JKT Queens ambayo ilikuwa inashiriki ligi ya kikapu mkoa wa Dar es salaam.

Mwakyembe amesema taifa limepoteza mtu muhimu aliyekuwa anajitoa kwaajili ya timu yake ya taifa kwa ujumla huku akitoa pole kwa familia pamoja na Jeshi la Kujenga Taifa.