Alhamisi , 18th Oct , 2018

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe leo ameteua wajumbe wapya watakaounda Bodi ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Harrison Mwakyembe kushoto na Mwana FA kulia

Uteuzi huo ambao umeanza tangu Oktoba 5, 2018, umetangazwa leo ikiwa ni siku 17 zimepita tangu Rais Dkt. John Magufuli alipomteua Bw. Habbi Gunze kuwa Mwenyekiti wa baraza hilo.

Kwa mujibu wa Katiba, waziri wa Wizara hiyo ana dhamana na anawajibika kuteua wajumbe wa Bodi baada ya Rais kumteua Mwenyekiti wake, ambapo leo waziri Mwakyembe amefanya hivyo huku akiwajumuisha wasaani wawili kati ya wajumbe hao watano.

Wasanii walioteuliwa miongoni mwa wajumbe hao ni msanii wa HipHop Hamis Mwinjuma maarufu Mwana FA, pamoja na muigizaji Single Mtambalike maarufu kama Richie.

Aidha, wajumbe hao wataitumikia bodi hiyo kwa muda wa miaka mitatu. Maelezo zaidi ya uteuzi huo yapo kwenye taarifa hapo chini.