Mwarabu aliyekabidhiwa Simba, anaogopesha

Jumatano , 13th Mar , 2019

Kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya wenyeji Simba SC dhidi ya AS Vita, wachezaji wa Simba wanatakiwa kuwa na nidhamu ya hali ya juu, kutokana na mwamuzi wa mchezo huo Noureddine El Jaafari kusifika kwa kumwaga kadi na kutoa penalti.

Refarii wa Morocco

Noureddine El Jaafari raia wa Morocco, ameteuliwa na CAF kuchezesha mchezo huo wa Jumamosi kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam ambapo refa huyo ni mkali awapo kwenye majukumu yake.

Akiwa tayari ameshachezesha mechi kadhaa za hatua ya makundi msimu huu, Noureddine El Jaafari ameshatoa jumla ya kadi 18. Kati ya hizo kadi za njano ni 16 na kadi nyekundu ni 2.

Moja ya mechi ambayo Noureddine El Jaafari alichezesha na kutoa kadi nyingi ni ile ya kundi C kati ya CS Constantine dhidi ya TP Mazembe ambao ulimalizika kwa Mazembe kupoteza kwa mabao 3-0 huku yeye akitoa kadci 4 za njano ikiwa ni mbili kwa kila timu.

Wachezaji wa Simba ambao wamekuwa wakipata kadi za njano ni pamoja na Jonas Mkude, Juuko Murshid, Cletous Chama, Paul Bukaba pamoja na Emmanuel Okwi, hivyo wanatakiwa kuwa waangalifu zaidi katika mchezo huo.