Alhamisi , 7th Nov , 2019

Klabu za Newcastle United na West Ham United zote za ligi kuu ya Uingereza EPL, zimeonesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Genk na timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta, kwa mujibu wa mtandao wa soka wa BBC Sport.

Goli la Mbwana Samatta

Hiyo imekuja baada ya kuonesha kiwango kikubwa katika mchezo wa marudiano wa Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Liverpool uliopigwa katika dimba la Anfield, ambapo Samtta alifunga bao safi la kichwa.

Kwa mujibu wa vipengele vya mkataba wake, klabu yoyote inayomtaka mshambuliaji huyo inatakiwa kutoa kiasi cha Pauni 10 milioni ili kumng'oa kwa mabingwa hao wa Ubelgiji.

Samatta (26) alikuwa mfungaji bora namba mbili wa ligi kuu ya soka ya Ubelgiji msimu uliopita, akifunga mabao 25 na msimu huu tayari amefunga mabao sita katika mechi 13 za mashindano yote alizocheza.