Jumapili , 20th Sep , 2020

12:30 za jioni hii leo, nyasi za uwanja wa Stamford Bridge zitakuwa zikiadhibiwa na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini Uingereza maarufu Premier League 'EPL' Majogoo Liverpool 'The Reds' watakaokuwa wageni wa matajiri wa jiji la London Chelsea 'The Blues'.

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp na kocha wa Chelsea, Frank Lampard

Michezo 186 kati ya matajiri wa jiji la London 'The Blues' Chelsea FC dhidi ya 'The Reds' majogoo wa jiji la Liverpool, Liverpool FC tayari imeshapigwa huku Liverpool wakiwa wababe kwa michezo 81 ya ushindi ilihali Chelsea wameshinda michezo 41 pekee huku michezo 64 wakitoka suluhu.

Rekodi zinaonesha Chelsea hadi sasa tayari wameshapoteza michezo mitatu ya mwisho dhidi ya Liverpool katika Ligi Kuu Uingereza EPL, rekodi hii inazidiwa na rekodi ya kupoteza michezo yao minne mfululizo dhidi ya majogoo hao Liverpool tangu Novemba 2010 hadi Mei 2012.

Michezo sita ya mwisho ya The Blues 2020-21 EPL ndani ya uwanja wake wa nyumbani Stamford Bridge wameibuka na ushindi, mara ya mwisho kuwa na mfululizo huu wa ushindi katika uwanja wa nyumbani ilikuwa ni 2017 chini ya Antonio Conte walipoibuka na ushindi mara saba mfululizo.

Jurgen Klopp amefanya uamuzi wa kumuingiza kundini kiungo wa timu ya taifa ya Uhispania Thiago Alcantara kwa dau la Euro milioni 20 kutoka Bayern Munich.

Kikosi kinachotegemewa kuanza hii leo kwa upande wa Chelsea ni pamoja na Kepa Arrizabalaga, Reece James, Antonio Rudiger, Kurt Zouma, Marcos Alonso, Ngolo Kante,Mateo Kovacic, Mason Mount, Kai Havertz, Timo Werner na Olivier Giroud.

Wakati mabingwa watetezi Liverpool wanategemewa kuwakilishwa na Alisson Becker, Alexander-Arnold, Joe Gomez, Virgil Van Dijk, Andy Robertson, Fabio Henrique 'Fabinho', Georginio Wijnaldum, Jordan Henderson, Mohamed Salah, Roberto Firmino na Sadio Mane.