Jumapili , 20th Mei , 2018

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Ujerumani Joachim Loew amekiri alifanya makosa ya kumlinganisha mchezaji taifa hilo Mario Gotze na mshamuliaji wa timu ya Barcelona, Lionel Messi  ambaye ni raia wa Argentina. 

Kwa mujibu wa jarida la michezo la Tencent Sports, Kocha huyo amesema hayo leo Mei 20, 2018 wakati akielezea sababu ya kutomjumuisha Gotze katika kikosi ambacho kitaiwakilisha Ujerumani katika mashindano ya kombe la Dunia Nchini

Urusi, Juni 14, 2018 na kuongeza kuwa aliamua kumfananisha Gotze na Messi ili kumtia moyo mchezaji huyo
“Sikufikiria athari ambayo angeweza kuipata kabla ya kusema maneno yale kwa Gotze, nilifanya vile kwa lengo la kumtia moyo lakini ilikuwa ni makosa kutamka hadharani, miezi michache baadae kauli ile ilianza kumaathiri Gotze,  hajacheza vizuri msimu huu, sio “super Mario” ambae tulikua tunamfahamu siku zote” amesema Loew.

Loew ameongeza kuwa kauli yake ilimbebesha mzigo mkubwa mchezaji huyo na hivyo kuanza kanza kushuka kiwango ingawa anaamini Gotze ni mchezaji bora na ataweza kurudi katika kiwango chake baada ya majira ya kiaangazi.

Mario Gotze aliiwezesha timu ya Taifa ya Ujerumani kushinda kombe la Dunia baada ya kufunga goli pekee katika dakika za nyongeza dhidi ya Taifa la Argentina katika mashindano ya kombe la Dunia yaliyofanyika nchini Brazil mwaka 2014.