Jumapili , 22nd Jul , 2018

Nyota wa klabu ya soka ya Arsenal na timu ya taifa ya Ujerumani Mesut Ozil ametoa ufafanuzi juu ya picha alizopiga mwezi Mei na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan, kwa kueleza kuwa hakuwa anaunga mkono mambo yake ya kisiasa bali ilikuwa ni masuala ya elimu.

Mesut Ozil

Ozil ambaye ni mzaliwa na Ujerumani mwenye asili ya Uturuki, amesema hawezi kupinga ukweli kuwa yeye amezaliwa na kuishi Ujerumani lakini asili ya familia yake ni Uturuki hivyo lazima atahusika tu kwenye masuala mbalimbali ya Uturuki ila lengo lake si kushiriki kuunga mkono yasiyofaa.

"Nina mioyo miwili, mmoja wa Kijerumani na mwingine Kituruki na mama yangu alinifundisha kuwa na heshima na kutosahau nilikotokea hivyo kupiga picha na Rais wa Uturuki haikumanisha naunga mkono masuala yake ya kisiasa lakini ni kuheshimu asili yangu'' - amesema.

Kushoto ni mchezaji Mesut Ozil akiwa na Rais Erdoğan.

Katika barua yake Ozil ameeleza kuwa vyombo vya habari hususani vya Ujerumani vimekuza tu suala hilo kutokana na Rais Erdoğan kuwafanyia ukatili baadhi ya wanahabari na wanasiasa wakati wa uchaguzi wa Rais nchini humo ambapo aliibuka mshindi.

Ozil na Erdoğan pamoja na mchezaji mwingine wa Ujerumani İlkay Gündoğan ambaye naye ana asili ya Uturuki walipiga picha ya pamoja mwezi Mei wakati Rais huyo alipotembelea Uingereza.